Mkazi wa Mwime wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Azard Ibrahimu amefikishwa katika Mahakama ya wilaya kwa tuhuma ya kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi gramu 30.5 kinyume cha sheria.
Mbele ya hakimu mkazi wa Mahakama hiyo Ushindi Swalo mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Peter Masau amesema Azard alitenda kosa hilo Agosti 6 mwaka huu katika eneo la mwime.
Amesema katika shauri hilo la jina namba 283 la mwaka huu mtuhumiwa amekiuka kifungu namba 17 (1) b (2) sura 5 ya sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya ya mwaka 2015.
Kwa upande wake Azardi amekana kutenda kosa hilo na shauri hilo limeahirishwa hadi agosti 23 mwaka huu litakapotajwa mahakamani hapo na upelelezi wake bado haujakamilika.
Dhamana ya Mtuhumiwa iko wazi kwa kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya shilingi milioni mbili kila mmoja na amepelekwa gerezani kwa kushindwa kutimiza mashariti hayo.
Social Plugin