DKT.GWAJIMA ATAKA WAGONJWA WANAOTUMIA CHF ILIYOBORESHWA WATHAMINIWE


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia afya Dk. Doroth Gwajima,akizungumza na watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa.
Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Chamwino,Dk.Zipora Mfugale,akizungumzia kuhusu jinsi walivyojipanga kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo wa CHF iliyoboreshwa na jinsi watakavyotoa ushauri kwa wananchi kujiunga na CHF iliyoboreshwa
Mratibu wa Ugharamiaji wa huduma za Afya-Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Boniphance Richard,akisisitiza jambo kwa watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu walipotembelea na kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia afya Dk. Doroth Gwajima,akitoa maelezo kwa watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akiwaonyesha kadi ya CHF iliyoboreshwa wananchi waliofika katika kituo cha Afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa huku akiwahimiza zaidi ili wajiunge na wapate huduma iliyobora.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika kituo cha Afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa huku akiwahimiza zaidi ili wajiunge na wapate huduma iliyobora.

*****

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia afya Dk. Doroth Gwajima, amewataka watumishi wa afya kote nchini kuacha kuwabagua au kutowapa kipaumbele wateja wanaotumia kadi za bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kwa kuwahudumia watu wenye fedha mkononi kwanza.

Dk. Gwajima ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa wilayani hapo.

Amewataka watumishi wa afya kuwapa kipaumbele wagonjwa wanaotumia kadi hizo ili kuweza kuongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo huo nchini.

Dk Gwajima Amewataka watumishi kote nchini kuendelea kuhamasisha matumizi ya kadi hizo ili kuongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo huo hapa nchini na watu wengi waweze kujiunga.

Amesema hivi sasa kadi za CHF iliyoboreshwa imefanyiwa marekebisho makubwa na serikali hali ambayo inamwezesha mgonjwa kupata huduma katika hospitali yoyote hadi ngazi ya mkoa.

Pia amewataka watumishi wa afya nchini kutoa huduma zenye ubora ili kuweza kuwavutia wananchi kujiunga na mifumo hiyo ya bima ya afya ya jamii.

"Kama tusipotoa huduma bora hivi vituo vyetu tulivyojenga nchi nzima vitakuwa havina maana lazima sisi kama watumishi wa afya tubadilike ili kuweza kuwavutia wananchi kuja katika vituo vyetu kupata huduma ya afya"

"Sitaki kusikia baada ya siku hizi 14 kuwa kuna kituo kimeshindwa kutuma taarifa zake au mifumo inakataa kwani kila kituo kinatakiwa kutuma taarifa zake za wateja waliohudumiwa ili kuweza kurejeshewa fedha zake ambazo zitatumika katika mahitaji mbalimbali ya eneo hilo"amesema Dkt Gwajima.

Naye mganga mfawidhi wa kituo cha afya Chamwino, Dk. Zipora Mfugale amesema kuwa wamejipa kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo wa CHF iliyoboreshwa.

Kwa upande wake ,Meneja Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya Ally-Kebby Abdallah,amesema kuwa Azma ya Serikali ni kutengeneza mfumo wa bima ambao mwananchi atatambuliwa lakini pesa anayochangia irudi kwenye kituo.
Hivyo ametoa raia kwa watumishi wa kituo cha Afya Chamwino kuwahamasisha wananchi wajiunge na CHF iliyoboreshwa kwa kushirikiana na uongozi wa sehemu husika. 

Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamechangia kwa kiasi kikubwa katika kuunda mfumo wa kutendea kazi wa IMIS na kutoa mafunzo kwa waandikishaji, waratibu na wasimamizi wa CHF Iliyoboreshwa nchini mpaka kufikia hapa.

Mradi wa HPSS utaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania hadi hapo CHF Iliyoboreshwa itakapo wafikia Wananchi wote wasio katika sekta iliyo rasmi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post