IRAN YAZINDUA RASMI MFUMO WA MAKOMBORA WA BAVAR-373


Rais Hassan Rouhani wa Iran amepongeza kuongezeka kwa nguvu ya nchi hiyo dhidi ya shinikizo linaloongezeka la Marekani, na kusema nchi yake haijawahi kusikitishwa kutokana na njama za adui, bali imesimama dhidi yao kwa nguvu zaidi.

Rais Rouhani amesema hayo katika hafla ya kuzindua mfumo wa makombora ya ulinzi wa anga aina ya Bavar-373 iliyofanyika jana. 

Amesema shinikizo la Marekani dhihi ya Iran limeshindwa, na kuwapongeza wataalam wa Iran kwa kusanifu na kujenga mfumo huo.

Waziri wa ulinzi wa Iran ambaye pia alihudhuria hafla hiyo Bw. Amir Hatami amesema Iran imefanikiwa kutengeneza mfumo makini ambao sio tu unakabiliana na matishio ya anga, bali pia unatambua, kufuatilia, na kuharibu ndege na makombora yanayoweza kukwepa rada.

Mfumo huo wa makombora una uwezo wa kulenga shabaha hadi umbali wa kilomita 65 angani na kupiga umbali wa karibu kilomita 300 za nchi kavu. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post