Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAJI MKUU WA TANZANIA KUONGOZA JOPO LA MAJAJI WATATU KUSIKILIZA MASHAURI 29 YA RUFAA IRINGA


Na Lusako Mwang’onda, Mahakama Kuu – Iringa
Jumla ya mashauri 29 yanatarajiwa kusikilizwa mkoani Iringa katika kikao maalum ‘session’ ya Mahakama ya Rufani chini ya jopo la Wahe. Majaji watatu likiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma.


Akizungumzia kuhusu kikao hicho ‘session’ mapema Agosti 19, 2019, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Eddie Fussi amesema kuwa katika kikao hicho kuna jumla ya mashauri ya rufaa za jinai ishirini na tano (25), rufaa za madai mbili (2) na maombi ya madai mawili (2)

Mhe. Fussi ameongeza kuwa kati ya mashauri hayo ishirini na tisa (29); matatu (3) ni ya zamani (backlogs) na ishirini na sita (26) ni ya muda wa kati na mapya (back stopping).

Kikao hiki cha Mahakama ya Rufani kilichoanza wiki iliyopita ni cha pili (II) kufanyika ndani ya mwaka huu. Majaji wengine waliopo katika jopo hilo ni pamoja na Mhe. Richard Mziray, Mhe. Rehema Mkuye na Mhe. Ignas Kitusi.

Kikao hicho kinatarajiwa kukamilika Agosti 30 mwaka huu na mara baada ya kukamilika kwa kikao hicho, Mhe. Jaji Mkuu anatarajia kufanya ziara ya kikazi kwenye Mahakama zote za mikoa ya Iringa na Njombe, ambapo atakagua maendeleo ya shughuli mbalimbali za kimahakama na kuzungumza na watumishi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com