Bunge la Uganda limepitisha sheria inayopinga hukumu ya adhabu ya kifo kwa baadhi ya uhalifu, na kufanya marekebisho katika sheria nne tofauti ikiwemo sheria ya kupambana na ugaidi.
Kama sheria hiyo itasainiwa na rais Yoweri Museveni , marekebisho hayo yatasitisha hukumu ya kifo kwa uhalifu mkubwa zaidi, kwa maelekezo ya jaji.
Watunga sheria wanasema kuwa hii ni hatua kubwa inayoweza kutokomeza hukumu hiyo, jambo ambalo mahakama iliwahi kupigia kelele.
Kuna wafungwa 133 ambao wamehukumiwa kunyongwa lakini sasa imepita miaka 20 tangu wahukumiwe.
Kumekuwa na kampeni mbalimali za kutokomeza hukumu hilo, kufuatia hukumu ya mwaka 2009 ya mfungwa Susan Kigula ambaye alihoji juu ya hukumu ya kifo kuwa kinyume na katiba.
Mahakama baadae ilitaka hukumu ya kifo isiwe lazima kwa kesi za mauaji, na kuwasisitiza watu kuwa mtu hapaswi kuwekwa jela kwa miaka mitatu wakati amehukumiwa kunyongwa muda huo ukipita mfungwa huyo ni sawa kuwa amepewa hukumu ya kifungo cha maisha.
Via BBC
Social Plugin