Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIJANA MBARONI KWA KUBAKA NA KUMPA MIMBA WANAFUNZI MWENYE UMRI WA MIAKA 17 KAHAMA

NA SALVATORY NTANDU

Mkazi wa mtaa wa Manzese wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Lazaro Mateyo (18) amefikishwa katika Mahakama ya wilaya kwa tuhuma ya kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi umri wa miaka (17).

Mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo Ushindi Swalo mwendesha mashitaka wa jeshi la Polisi Peter Masau amedai kuwa Lazaro alitenda kosa hilo mwezi April mwaka huu katika mtaa huo.

Amesema Mshitakiwa baada ya kutenda makosa hayo alitoroka kusiko julikana hadi alipokamatwa na polisi Agosti hii na kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili kwa mujibu wa sheria.

Katika shauri hilo la jinai namba 281 la mwaka huu Lazaro anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi huyo kinyume na kifungu namba 130 (1) na (2) 132  vya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002.

Kosa la pili anatuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi huyo kinyume na kifungu cha 60 (1) sura 133 cha sheria ya elimu ya mwaka 2016.

Kwa upande wake Lazaro amekanamashitaka hayo na shauri hilo limeahirishwa hadi Agosti 23 mwaka huu na dhamana ya mshitakiwa ipo wazi kwa kuwa na wadhamini wawili ambao watatakiwa kulipa bondi ya shilingi milioni mbili kila mmoja.

Mshitakiwa ameshindwa kutimiza mashariti ya dhamana na amepelekwa gerezani na upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com