Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KOREA KASKAZINI YAFYATUA KOMBORA JINGINE LA TATU


Korea kaskazini imefyatua kombora la masafa mafupi ambalo halijabainika mara mbili , kwa mujibu wa maafisa wa Korea Kusini , katika jaribio la tatu la silaha hizo katika kipindi cha wiki moja pekee.

Ufyatuaji wa makombora hayo ulifanyika katika eneo la mwambao wa mashariki mwa taifa hilo mapema Ijumaa.

Hatua hiyo inaonekana kama hatua ya taifa hilo inayolenga kujibu mazoezi ya kijeshi ya baina ya Korea Kusini na Marekani yanayotarajiwa kuanza mwezi huu.

Wakati huo huo Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeitaka Korea kaskazini kushiriki mazungumzo ya "maana " na Marekani.

Baada ya mkutano wa faragha katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa , mataifa yalisema kuwa vikwazo vya kimataifa vinapaswa kuimarishwa hadi utawala wa Pyongyang utakapoangamiza mipango yake ya nyuklia ya makombora ya masafa.

Ufyatuaji wa makombora hayo ulifanyika katika eneo la Yonghung katika jimbo la South Hamgyong katika bahari ya Japan, inayofahamika pia kama Bahari ya Masharik , kwamujibu wa Mkuu wa kikosi cha pamoja cha Korea kaskazini na Korea Kusini (JCS).

Eneo hilo linaonekana kama kituo cha kufyatulia makombora ambacho hakijawahi kutumiwa awali , amesema Ankit Panda, afisa katika shirikisho la wanasayansi wa Marekani - Federation of American Scientists.

"Hiki ni kielelezo kingine cha enzi ya Kim Jong-un zaidi ya ufyatuaji wa makombora ya usiku : kufyatua kutoka vituo ambavyo havikuwahi kutumiwa awali au ambavyo havitumiwi"

Akizungumza katika ikulu ya White House, rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hana hofu na ufyatuaji wa hivi karibuni wa  makombora kwasababu ni ya masafa mafupi na "ni ya kiwango cha kawaida ".



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com