Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KOREA KASKAZINI YAPUUZA MAZUNGUMZO YA NYUKLIA NA MAREKANI


Korea Kaskazini imesema haioni manufaa ya majadiliano hadi Marekani isitishe kile ilichokiita hatua za uhasama za kijeshi, wakati mjumbe wa Marekani akizuru Korea Kusini kwa jicho la kufufua mazungumzo ya nyuklia na Pyongyang. 

Mazungumzo kati ya Pyongyang na Washington yamekwama, tangu mkutano wa pili wa kilele kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mjini Hanoi Februari, ulipovunjika bila makubaliano. 

Wawili hao walikutana tena mwezi Juni katika ukanda wa amani kati ya Korea mbili na kukubaliana kuanzisha tena majadliano ya ngazi ya kikazi, lakini mazungumzo hayo bado kuanza. 

Wakati huohuo, Korea Kaskazini imefanya majaribio kadhaa ya makombora ya masafa mafupi katika wiki za karibuni, kupinga mazoezi ya  kijeshi ya kila mwaka kati ya Marekani na Korea Kusini, ambazo inaziona kama mazoezi ya kujiandaa na uvamizi. 

Stephen Biegum, mjumbe maalumu wa Marekani kwa ajili ya Korea Kaskazini, anaeongoza mazunguzo ya kikazi, aliwasili Seoul Jumanne jioni kwa ziara ya siku tatu, na alisema Washington itakuwa tayari kushiriki mazungumzo mara itakaposikia kutoka Pyongyang.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com