Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LORI LA MAFUTA LATEKETEA KWA MOTO KAHAMA NA KUSABABISHA KIFO CHA UTINGO HUKU DEREVA AKIJERUHIWA

NA SALVATORY NTANDU
Lori lenye shehena ya mafuta la kampuni ya Mount Meru Company  limeanguka na kuwaka moto   wilayani kahama mkoani Shinyanga  na kusababisha kifo cha utingo wa lori hilo aliyefahamika kwa jina moja la Erik huku dereva wake Ibrahimu Issa  akijeruhiwa kwa moto.

Lori hilo lenye namba za usajili RAD 416V na Tela namba RL 1950 likitokea Dar es laam likiekea nchini Rwanda likiendeshwa na Ibrahim Issa limepata ajali hiyo katika mtaa wa shunu usiku wa kuamkia leo na kulipuka wakati likikwepa gari dogo aina ya Toyota Voltz.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa mtaa wa shunu, Kube Shija amesema baada ya tukio hilo kutokea alitoa taarifa kwa jeshi la polisi na walifanikiwa kuwazuia wananchi ambao walitamani kwenda kuiba mafuta lakini walifanikiwa kuwazuia.

Amesema ni vyema wananchi wakajifunza kutokana na majanga ya moto kama vile ajali ya morogoro ambapo watu wengi wamefariki dunia kwa kutokimbilia magari ya mafuta pindi yapo anguka ili kuzuia madhara kama vile vifo.

Frank kalebela na Asha Hamisi ni baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo  wamesema ni vyema serikali ikatoa elimu juu ya majanga ya moto ili kuzuia vifo visvyokuwa vya lazima ambavyo vinasababishwa tamaa za kujipatia mali.

Ibrahimu Mussa ni dereva wa lori hilo ambaye anapatiwa matibabu katika hospiali ya Halmashauri ya mji wa kahama amesema ajali hiyo imetokea wakati akimkwepa dereva wa gari dogo ambaye alikuwa anajaribu kupita bila kuchukua tahadhari  na kusababisha gari hilo kuanguka.

Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji wilaya ya kahama  Dumma Mohamed  amesema walifanikiwa kuuzima moto huo na kumwokoa dereva wa gari hilo ambaye mpaka sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama

Amewataka  wananchi kutoa taarifa za majanga ya moto na kuacha tabia ya kupiga picha na kuzisambaza mtandaoni ili kuweza kuokoa mali za watu pindi moto unapotokea.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani shinyanga  ACP Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa ajali.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com