Wakazi katika kijiji cha Rodoma, Kieni, Kaunti ya Nyeri nchini Kenya wamekumbwa na mshtuko mkubwa baada ya watu wanne kuaga dunia baada ya kula chakula kinachodaiwa kuwa na sumu kwenye sherehe ya posa.
Familia hiyo ilikutana katika kijiji cha Rodoma, Kaunti ya Nyeri kwa ajili ya sherehe ya kulipa mahari.
Miongoni mwa waliopoteza maish ni mama ya bwana mtarajiwa na wakwe wawili huku watu wengine kadhaa waliokula chakula kwenye sherehe hiyo wakilazwa hospitalini.
Akizungumza na Citizen TV Jumatatu, Agosti 19,2019 Naibu Kamishna wa Kaunti ya Kieni Magharibi Samuel Kariuki alithibitisha kisa hicho na kusema wanne waliaga dunia na wengine kupelekwa hospitalini.
Kulingana na Kariuki na wengine waliokuwa na ufahamu kuhusu mkasa huo, waliopika chakula hicho ni wapishi waliokodishwa kutoka soko la Gikomba, Nairobi.
Baadhi ya walioaga dunia walidaiwa kuumwa na tmbo na kuendesha na wageni wengine walikimbizwa katika zahanati ya Kariminu baada ya kuanza kuhisi maumivu makali.
Social Plugin