Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWENYEKITI WA KITONGOJI AUAWA KWA MAPANGA KAHAMA ,USHIRIKINA WA RADI ILIYOUA WAWILI WAHUSISHWA


Na Salvatory Ntandu 
Watu wasiojulikana wamemvamia na kumuua papo hapo Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyambula kata ya Ngogwa, Halmashauri ya mji wa Kahama Hamisi Kadilanha Salehe(58) kwa kumkata na kitu chenye ncha kali wakati akiwa amelala na mkewe Shija Mkela Maziku(45).

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea Agosti 6,2019 majira ya saa mbili usiku  ambapo watu hao wapatao watano walitekeleza mauaji hayo na kisha kumjeruhi Shija Mkela Maziku.

"Chanzo cha tukio hilo kinasadikiwa ni imani za kishirikina 
kutokana na tukio la kupigwa na radi mwezi wa Februari, 2019 ambapo ilisababisha kifo cha mdogo wake na marehemu aitwaye Mhoja  S/O Kadilanha Salehe (45), mkazi wa Nyambula pamoja na mkewe aitwaye Pili Tabu Mabula (36),mkazi wa Nyambula na wakati wengine waliokuwa pamoja nao hawakupata madhara kutokana na radi hiyo",ameeleza.
Amefafanua kuwa, mbinu iliyotumika ni kuvunja mlango na kumvamia akiwa amelala chumbani kwake na mkewe nakuongeza mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Halmashauri Mji wa Kahama.

Kamanda Abwao amesema katika tukio hilo watu hao waliwajeruhi watu wawili ambao ni mke wa marehemu Shija Maziku na Dada yake Pili tabu Mabula ambao wote wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Halmashauri ya mji.

Ameongeza kuwa jeshi la polisi kwa kushirikina na wananchi linaendelea kuwatafuta watu hao walifanya mauaji na watakapobainika watachukuliwa hatua za kisheria kama ambavyo wamekuwa wakichukuliwa watu wengine wanaojichulia sheria Mkononi.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com