Mawakili wanne wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala watamtetea Tundu Lissu katika kesi ya kupinga kuvuliwa ubunge. Lissu anaiomba mahakama ibatilishe yeye kuvuliwa ubunge, izuie Mbunge Mteule, Miraji Mtaturu kuapishwa, na kuamuru Bunge kumlipa stahiki zake zote wakati akitibiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Alute Mughwai ambaye ni kaka yake Lissu amesema kesi hiyo itaanza kuunguruma Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Mbali na Kibatala, mawakili wengine ni Jeremia Mbesya, John Malya na Fredi Kalonga.
Amebainisha kuwa maombi ya kufunguliwa kesi hiyo chini ya hati ya dharura, kupitia kwake (Mughwai) aliyempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo, yatasikilizwa Agosti 21, 2019.
Social Plugin