Mbunge wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu ambaye ni mashuhuri zaidi kwa jina la Bobi Wine ameshtakiwa kwa kosa la kumkasirisha na kumkejeli Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.
Mbunge huyo na wenzake wanatuhumiwa pia kuurushia mawe msafara wa Rais Yoweri Museveni wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi katika mji wa kaskazini wa Arua mwaka uliopita wa 2018.
Aidha shitaka hilo jipya limeongezwa katika orodha ya mashtaka mengine yanayomkabili Mbunge huyo wa upinzani likiwemo lile la uhaini.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, iwapo Bobi Wine atapatikana na hatia atakabiliwa na kifungo cha maisha jela.
Bobi Wine bado anakabiliwa na mashtaka katika mahakama nyingine kwa kuongoza maandamano dhidi ya sheria inayoweka kodi katika mitandao ya kijamii pamoja na biashara zinazofanywa kupitia malipo ya simu za mkononi.
Halikadhalika, Mbunge hivi karibuni alitangaza nia yake ya kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao.
Social Plugin