NA Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendelelo (CHADEMA) Mh Wilfredy Muganyizi Rwakatale amempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuri kwakuendelea kukarabati meli ya abiria na mizigo itakayokuwa inafanya safari zake Bukoba-Mwanza.
Mh Rwakatale amesema hayo katika mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo la Bukoba Mjini uliofanyika August 7 2019 katika kata ya Hamugembe manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wenye lengo la kuzungumzia miradi mbalimbali ya kimaendeleo iliyofanyika kwa kipindi cha miaka minne kwenye uongozi wake wa jimbo na kuongeza kuwa jitihada za ukarabati wa meli hiyo unaendelea kwa kasi chini ya uongozi wa awamu ya tano unaoongozwa na Dk John Magufuri.
Aidha mh Rwakatale amewataka wananchi wa mkoa wa Kagera ususani jimbo lake la manispaa ya Bukoba kuwa na subira katika kipindi hiki ambapo meli inaendelea kutengenezwa na itakapo kuwa imekamilika itawaondolea usumbufu wa kuendelea kusafiri kwa kutumia mabasi kwenda mkoani Mwanza.
Katika miaka minne ya uongozi wake mh Rwakatale ameweza kutekeleza miradi mbalimnbali ya kimaendeleo katika jimbo lake ikiwemo kuchangia shilingi milioni 16 kuwezesha ukarabati wa uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kashai, mabati 56 kwa ajili ya kuezeka shule ya msingi Nyamkazi, ametoa shilingi milioni 2 kila kata kwenye kata 14 ili kuwezesha utengenezwaji wa madawati na mengine mengi.
Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh Conchesta Rwamulaza amewaomba wananchi wa mkoa wa Kagera kujitokeza katika kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura ili waweze kushiriki katika ushaguzi wa serikari za mitaa utaotarajia kufanyika mnamo mwaka huu.
Mh Rwamulaza ameongeza kuwa ili wananchi wapate kiongozi bora inabidi washiriki katika zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura ambapo zoezi ilo kwa upande wa mkoa wa kagera limetajwa kuanza kufanyika mnamo mwezi wa tisa mwaka huu.
Social Plugin