Watu kadhaa wamekufa baada ya lori la mafuta kulipuka jana kwenye mtaa wa Rubirizi, magharibi mwa Uganda.
Msemaji wa polisi wa mkoa wa Great Bushenyi, Marshal Tumusiime, amesema, mlipuko huo ulitokea baada ya lori hilo kupinduka, kulipuka na kuwaka moto katika kituo cha biashara cha Kyambura, kando na Barabara kuu ya Kasese-Mbarara.
Moto huo ulienea katika nyumba na maduka kadhaa na kuteketeza vitu. Onesmus Nkesiga ambaye duka lake lilikumbwa na moto huo, alisema amepoteza bidhaa zenye thamani ya USh 20 milioni.
Wazima moto ambao walifika katika eneo hilo saa moja baada ya tukio, wameokoa vitu kadhaa kwenye baadhi ya maduka.
Social Plugin