Mwekezaji wa simba SC Mohamed Dewij amefunguka na kuonyesha jinsi alivyoumizwa na matokeo mabaya ya timu ya Simba dhidi ya wapinzani wao kutoka Msumbiji UD Songo katika michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kutolewa mapema kwenye michuano hiyo
Hii imekuja baada ya Simba kupata sare ya 1-1 wakati mchezo wa kwanza nchini msumbiji matokeo yalikuwa 0-0, hivyo goli la ugenini liliwabeba UD Songo na Simba kutupwa nje ya michuano licha ya msimu uliopita kufanya vizuri kwa kufika hatua ya robo fainali.
Kupitia kiurasa zake za mitandao ya kijamii Mo Dewij ameandika hivi:-
Wanasimba, mnisamehe kwa ukimya. Maumivu ya matokeo yametupata sote. Naomba tukumbushane: Sisi ni SIMBA! Simba lazima anyanyuke! Hawezi kukata tamaa.
Niwaombe tusivunjike moyo wala kukata tamaa. Hatutaogopa maneno ya watu na hatutaacha kupambana na kujipanga kwa ajili ya malengo yetu. Msimu huu tutautumia kikamilifu kuhakikisha tunaboresha mipango yetu ili msimu ujao turudishe furaha kwa Wanasimba wote.
Tumwombe Mwenyezi Mungu atutangulie katika safari yetu endelevu. Tukumbushane tena: Roma haikujengwa kwa siku moja. Tuwe wavumilivu, tutafika tu Insha’Allah. 🙏🏽
Social Plugin