Mrembo atakayeshikilia taji la Miss Tanzania 2019, anatarajiwa kupatikana leo katika kilele cha mashindano hayo katika ukumbi wa Millenium Tower, Makumbusho, Dar es Salaam.
Shindano hilo linawakutanisha warembo 20 kutoka kanda sita ambazo ni Nyanda za Juu Kusini, Kati, Mashariki, Ziwa, Dar es Salaam na Vyuo Vikuu.
Katika upande wa zawadi, mshindi atapewa shilingi 10,000,000.
Majaji wa shindano hilo ni Angela Damas (Miss Tanzania 2002), Shyrose Banji, Kenned The Remedy (Mtangazaji), Miriam Ikoa na David Minja.
Social Plugin