Mahakama ya Wilaya ya Babati Manyara, imemuhukumu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Rift Valley Charles Msele,kifungo cha Maisha jela,kuchapwa viboko 4 na fidia ya Tsh. Million 3 kwa kosa la kuingia bweni la kiume na kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 11 anayesoma darasa la 5 shuleni hapo.
Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya Hakimu Simon Kobero, amesema adhabu hiyo imetolewa baada ya mtuhumiwa kutiwa hatiani.
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo September 28 mwaka jana.
Mtuhumiwa alimuita mtoto huyo bwenini na baada ya hapo na yeye alienda akiwa na vilainishi ambapo baada ya kufika bwenini mtuhumiwa alimpaka mafuta kwenye sehemu za haja kubwa kisha na yeye kujipaka na kumlawiti.
Upande wa mashtaka alisema kwa kuwa mshtakiwa ametiwa hatiani, mwendesha mashtaka Wakili wa serikali Petro Ngassa, aliomba mtuhumiwa apewe adhabu kali pamoja na kutoa fidia kwa muhanga kutokana na kitendo alichokifanya.
Social Plugin