Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Rashid Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema kutokana na mwili wa marehemu kuharibika vibaya, haikuweza kubainika moja kwa moja chanzo cha kifo chake.
Kwa upande wake Stephano Robart Makofia, ambaye ni mzazi wa marehemu amesema, alipofika eneo la tukio alimtambua mtoto wake kwa mavazi aliyokuwa amevaa siku aliyotoweka nyumbani.
Baadhi ya majirani wameitupia lawama familia hiyo, kwa madai walikuwa hawamjali mtoto wao.
Aidha Kamanda wa Polisi ametoa Rai kwa wazazi mkoani Katavi kuwa makini na watoto wao ili kuepuka majanga kama hayo kuwakuta watoto.
Chanzo - EATV
Social Plugin