Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
MARAISI wastaafu wa Serikali ya Tanzania wamehudhuria Mkutano Mkuu wa 39 unaofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kushuhudia Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk.John Magufuli akikabidhiwa Uenyekiti wa jumuiya hiyo.
Katika mitandao ya kijamii baadhi ya watu wasiokuwa na njema walikiwa wakizusha kuwa Dk.Magufuli amesusiwa mkutano huo na watangulizi wake.Hata hivyo uzushi wao umekosa mashiko kwani viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo marais hao wote wastaafu wamehudhuria mkutano huo wa kihistoria.
Marais wastaafu ambao wamehudhuria ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye ni Rais ww Serikali ya Awamu ya Pili,Benjamin Mkapa ambaye ni Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu,Jakaka Kikwete aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne na kwa upande wa Zanziabar Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Amani Karume.
Mbali ya wastaafu hao kuwemo kwenye mkutano huo ambao pia wametambulishwa kwa wageni mbalimbali kutoka nchi 15 za jumuiya hiyo,pia viongozi wengine wa Serikali ya Tanzania waliohudhuria ni Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Balozi John Kijazi,mawaziri, viongozi wa ngazi mbalimbali wastaafu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda.Pia wamehudhuria watu mashuri wa ndani na nje ya Tanzania.
Pamoja na shughuli mbalimbali ambazo zinaendelea kwenye mkutano wa jumuiya hiyo ambao utafanyika kwa siku mbili,tukio ambalo linasubiriwa na Watanzania wengi ni kuona Rais Dk.Magufuli anakabidhiwa Uenyekiti wa SADC.
Nafasi hiyo ya Uenyekiti wa SADC kwa Tanzania mara ya mwisho ilishikiliwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa miaka 16 iliyopita na sasa anakwenda kukabidhiwa Rais mchakazi Dk.Magufuli.
Hata hivyo nchi mbalimbali za jumuiya hiyo zimeonesha matumaini na imani kubwa kwa Rais Magufuli hasa kutokana na utendaji wake tangu akiwa Rais ambaye anaamini katika wananchi kufanya kazi na nchi kujitegemea.
Pia amekuwa na kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda ambayo itaipeleka nchi uchumi wa kati.Kwa nchi za SADC moja ya mkakati wao ni kuhamasisha viwanda kwa nchi wanachama kazi ambayo Rais Magufuli ameianza kabla ya kukabidhiwa uenyekiti,hivyo nchi za jumuiya hiyo zinaamini akiwa Rais Magufuli atawafikisha kwenye nchi ambazo uchumi wake utatokana na viwanda.
Social Plugin