Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog Bukoba
Shule ya msingi Ngarama iliyopo katika kata ya Katoro Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera iliyoanzishwa mwaka 1936 inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vyumba za walimu, madarasa na vyoo huku ikielezwa kuwa jamii haina uelewa juu ya masuala ya elimu shuleni hapo.
Akizungumza na Malunde1 blog, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ngarama, Pius Pancras leo Agosti 6 2019, amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 392 ambapo wavulana ni 195 wasichana197 shule inakabiliwa na ukosefu wa nyumba za walimu kwani kuna nyumba mbili moja imechakaa na nyingine inahifadhi walimu wawili huku wengine wakiishi mbali na shule hiyo.
Amezitaja changamoto zingine kuwa ni ukosefu wa vyoo, maji ya kunawa na kunywa huku ukosefu wa vyumba vya madarasa ukisababisha baadhi ya wanafunzi kusomea chini miti.
Ameeleza kuwa mbali na jamii kutokuwa na uelewa katika masuala ya elimu lakini pia hali duni ya kipato kwa wana jamii imechangia kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya wazazi kutompa ushirikiano Mwalimu huyo hasa pale anapowashirikisha katika masuala ya kupata lishe shuleni hapo.
Amesema hata kile ambacho kinaonekana shuleni hapo ni juhudi zake za mapambano huku akidai sasa amekata tamaa sasa amechoka kupambana peke yake kwani pamoja na kutoa kilio cha changamoto zinazoikabili shue hiyo kwa serikali kila inapotimia muda wa kutoa ripoti lakini hapati mafanikio.
"Mimi kinachoninyima usingizi ni hali hii ya shule licha kuwa taarifa ishatolewa lakini sioni kinachoendelea naomba serikali isaidie kupunguza changamoto hizi ili watoto wetu wapate elimu ili kukamilisha ndoto zao",amesema.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ngarama, Pius Pancras akielezea changamoto zinazoikabili shule hiyo.
Social Plugin