Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

OMBI LA BURUNDI KUJIUNGA NA JUMUIYA YA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA (SADC) LAKATALIWA


Ombi la nchi ya Burundi kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), limegonga mwamba baada kutokamilisha vigezo katika baadhi ya maeneo.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Agosti 18 na Rais Dk. John Magufuli wakati akihitimisha mkutano huo wa siku mbili ulioanza jijini Dar es Salaam jana.

Aakizungumzia hatua liyofikiwa kuhusu nchi hiyo kuweza kujiunga, amesema ilibainika kuwa bado kuna maeneo ambayo hayajakamilika vizuri.

“Mkutano umeielekeza sekretarieti kuiarifu Burundi kuhusu maeneo ambayo hayajakamilika ili yafanyiwe kazi na hatimaye kutumwa tena kwa timu ya uchunguzi  kwa ajili ya hatua nyingine za baadaye,” amesema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com