Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, amefanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua katika kata ya Masengwa na Samuye zilizopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuwaonya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakikwamisha wananchi kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.
Mboneko amefanya ziara hiyo leo Agosti 28, 2019 kwa akianzia wenye Kata ya Masengwa ambapo mkutano wake wa hadhara ameufanyia kwenye kijiji cha Bubale, huku kata ya Samuye akifanyia kwenye kijiji cha Ibingo.
Akizungumza kwenye mikutano hiyo, Mboneko aliwataka wananchi washiriki na kuchangia shughuli za maendeleo, na kuwapuuza watu ambao hupinga maendeleo.
Alisema Serikali itaendelea kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo zinawakabili likiwamo suala la maji, huduma za afya, umeme, kilimo, miundombinu ya barabara pamoja na elimu.
“Licha ya serikali kuendelea kutatua kero mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi, pia tunawaomba na nyie wananchi muwe mnashiriki kuchangia shughuli za maendeleo ili kuunga juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo, na muwapuuze wale ambao hupenda kupinga maendeleo,”alisema Mboneko.
“Naomba pia viongozi wa maeneo haya husika, pamoja na Diwani mtusaidie kutuletea majina ya watu ambao hupenda kupinga maendeleo na kukwamisha wananchi wasishiriki kuchangia shughuli za maendeleo ili tushughulike nao,” aliongeza.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao utafanyika Novemba 24 mwaka huu,Mboneko aliwataka wananchi wasichague viongozi wasiopenda maendeleo, bali wachague wale ambao ni wapigania maslahi ya wananchi ili wapate kutatuliwa matatizo yao.
Katika hatua nyingine amewataka maofisa ugani kuwatembelea wakulima na kuwapatia elimu ya kilimo cha kisasa, ili pale watakapoanza kulima walime kilimo chenye tija, ambacho kitawapatia mavuno mengi na hatimaye kuinuka kiuchumi.
Nao baadhi ya wananchi walioshiriki kwenye mikutano hiyo ya hadhara ya mkuu huyo wa wilaya, wamepongeza kwa kusikilizwa kero zao pamoja na kutatuliwa, yakiwemo masuala ya umeme, maji, barabara, elimu, pamoja na kilimo hasa kwenye ununuzi wa pamba.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza na wananchi wa kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuwataka washiriki kuchangia kwenye shughuli za maendeleo, licha ya serikali kuwatatulia matatizo yao ambapo nao wanatakiwa waunge juhudi hizo za serikali. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akionya watu ambao wamekuwa wakipinga maendeleo pamoja na kuwashawishi wananchi wasishiriki kuchangia shughuli hizo za maendeleo kuwa serikali itawachukulia hatua kali.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, akiwataka wananchi kuendelea kuiamini serikali yao ambayo ni sikivu ambapo itaendelea kutatua changamoto zao zote ambazo zinawakabili.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe.Jasinta Mboneko akizungumza pia na wananchi wa Kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuwataka washiriki kuchangia kwenye shughuli za maendeleo, licha ya Serikali kuwatatulia kero hivyo nao wanatakiwa waunge juhudi hizo za Serikali.
Diwani wa Kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemas Simoni, akiwahakikishia wapiga kura wake kuwa changamoto zao zote zitatatuliwa ikiwa serikali ya awamu ya awamu ya Tano ipo kwa ajili ya wananchi.
Diwani wa Kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga John Ngegeshi akiomba serikali kuongeza msukumo wa ukamilishaji wa mradi wa maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria pamoja na kasi ya usambazaji wa umeme wa REA.
Mtendaji wa Kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Husein Majaliwa akisoma taarifa ya kata hiyo na kueleza changamoto ambazo zinawakabili wananchi, ikiwemo uhakika wa masoko ya mazao yao ambayo hulima likiwemo zao la pamba.
Mtendaji wa Kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Damiani Ndassa, akisoma taarifa ya kata hiyo na kuelezea changamoto ambayo ipo ni wananchi kugoma kuchangia shughuli za maendeleo mara baada ya serikali ya Kijiji cha Ibingo kufanya ufujaji wa fedha.
Awali Mwananchi Jumanne Makanga mkazi wa kata ya Masengwa akiwasilisha kero kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bubale kata ya Masengwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Eliakimu Methew akiwasilisha kero kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Mwananchi Ndeshema Nshimbi mkazi wa Kata ya Samuye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwasilisha kero kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Kaimu Meneja wakala wa maji mijini na vijijini (RUWASA) Emaeli Nkopi, akijibu maswali ya ukamilishwaji wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya Jasinta Mboneko wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwenye Kata ya Masengwa na Samuye.
Msimamizi wa umeme wa REA Hally Twaha akimwakilisha Meneja wa Tanesco mkoa wa Shinyanga, akijibu maswali ya umeme kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Meneja wa TARURA halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Eng. Salvatory Yambi, akijibu maswali ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
DR Joseph Ngowi akimwakilisha Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Amosi Mwenda, akijibu maswali ya sekta ya afya yaliyoulizwa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi
Afisa ushirika wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akijibu maswali ya Pamba yaliyoulizwa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwenye Kata zote za Masengwa na Samuye.
Wananchi wa Kata ya Masengwa wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa.
Wananchi wa Kata ya Masengwa wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa.
Wananchi wa Kata ya Masengwa wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa.
Wananchi wa Kata ya Samuye wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa.
Wananchi wa Kata ya Samuye wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa.
Wananchi wa Kata ya Samuye wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa.
Wananchi wa Kata ya Samuye wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wa kusikilizwa kero zao na kutatuliwa.
Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog