Marais wawili, Edgar Lungu wa Zambia na João Manuel Gonçalves Lourenço wa Angola wamewasili Tanzania kuhudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mkutano huo unaoshirikisha nchi 16 za SADC unafanyika kuanzia kesho Jumamosi jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wa mkutano huo ni Rais John Magufuli wa Tanzania.
Marais wengine waliokwisha kuwasili nchini ni; Danny Faure wa Shelisheli na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini.
Social Plugin