Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Ocitti akiwaongoza wageni wake ,Balozi wa Uingereza nchini Tanzania ,Sara Cooke na Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha Biashara ,Andrew Rosindell walipotembelea kiwanda cha Bia cha Serengeti Moshi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Ocitti (wa pili kushoto)
akiwa na wageni wake ,Balozi wa Uingereza nchini Tanzania ,Sara Cooke (wa kwanza kulia)
na Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha Biashara ,Andrew
Rosindell wakijiandaa kuotesha miti katika kiwanda cha Bia cha Serengeti -Moshi.
Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha Biashara ,Andrew
Rosindell akizungumza wakati wa zoezi la kuotesha miti katika kiwanda cha Bia cha Serengeti ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa kuotesha miti katika mkoa wa Kilimanjaro .
Balozi wa Ungereza nchini Tanzania ,Sara Cooke akiotesha mti katika kiwanda cha Bia cha Serengeti mjini Moshi .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti ,Mark Ocitti akimwagia maji mti alioutosha katika kiwanda cha Bia cha Serengeti cha mjini Moshi ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuotesha miti 1000 katika mkoa wa Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Ocitti (kulia )akiwa na wageni wake ,Balozi wa Uingereza nchini Tanzania ,Sara Cooke (kushoto)
na Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha Biashara ,Andrew
Rosindell(katikati)
Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV
KATIKA kukabiliana na uharibufu wa Mazingira pamoja na
mabadiliko ya tabia nchi Kampuni ya Bia ya Seerengeti (SBL) kwa kushirikiana na
taasisi ya The Kilimanjaro Project wamezindua kampuni ya kuotesha miti 1000 kwa
mkoa wa Kilimanjaro.
Zoezi la uoteshaji miti linakuja huku kukiwa na wito kutoka
jumuiya ya kimaitafifa juu ya kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa kuongeza
juhudi za uhifadhi wa misitu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa
kuweka mazingira katika hali ya usalama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Akizungumza mara baada ya zoezi la kuotesha miti katika
kiwanda cha SBL kilichopo Pasua katika wilaya ya Moshi ,Mkurugenzi Mtendaji wa
SBL ,Mark Ocitti amesema SBL imeamua kuongeza jitihada za uhifadhi wa mazingira
sit u katika maeneo yaliyo chini ya SBL bali katika maeneo mbalimbali nchini
Tanzania.
“Huu ni uthibitisho tosha kwamba SBL imejidhatiti na iko
tayari kushirikiana na wadau wengine katika kutekeleza miradi yenye kuleta tija
kwa jamii zetu”alisema Ocitti.
Zoezi la uoteshaji miti limehudhuriwa na ujumbe kutoka
British High Commission akiwemo Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo
cha Biashara Andrew Rosindell pamoja na Balozi wa Uingereza nchini
Tanzania Sara Cooke waliotembea kiwanda
cha Bia cha Serengeti Moshi .
Mpango wa SBL unaenda sambamba na sera ya kampuni hiyo
katika kurudisha kwa jamii sehemu ya faida na umejikita zaidi katik autoaji wa
huduma bora ya maji safi kupitia mradi uitwao Water of Life (WOL) .
Mpango mwingine ilionao SBL ni pamoja na kuwasaidia
wanafunzi kupata ufadhili wa masomo ya elimu ya juu,kuwasaidia wakulima wa
ndani husuani wa vijijini pamoja na mpango wa kuhamasisha unywaji pombe
kistaarabu.
Mwisho .
Social Plugin