Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangala amesema Serikali itaanza kuuza asilimia 10 ya mamba nje ya nchi kwa kile alichokieleza kumekuwa na ongezeko kubwa sana, wanyama wakali kuingia kwenye makazi ya watu.
Waziri amesema Serikali imejhitahidi vya kutosha kuhakikisha suala la ujangiri linaisha na nchini na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa bali changamoto iliyopo, ni wanyama hao kuingia kwenye makazi ya watu.
Aidha, Kigwangalla amesema Serikali itauza viboko wote waliopo kwenye maziwa, mabwawa na mito yaliyopo maeneo ya mijini.
Kigwangalla ametaja miongoni mwa maeneo ambayo yana viboko watakaouzwa ni Mpanda, Mafia, Babati na kwamba mauzo hayo yatafanyika kwa mnada kwa utaratibu ambao utatangazwa wiki ijayo
Social Plugin