TETESI ZA SOKA LEO IJUMAA AGOSTI 23,2019

Alexis Sanchez
Manchester United itakabiliwa na deni la mshahara la pauni milioni 12 kwa mchezaji Alexis Sanchez hata kama atasajiliwa na klabu ya Inter Milan. (ESPN)

Sanchez, 30, ambaye ni raia wa Colombia alikosa mazoezi ya Alhamisi na klabu yake ya Man United baada ya kwenda ubalozi wa Marekani jijini London. (Sun)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 28, na mlinzi raia wa England James Tomkins, 30, wapo katika mazungumzo ya kuongeza mikataba yao na klabu ya Crystal Palace. (Guardian)

Barcelona wamekataa ofa ya klabu ya Inter Milan ambao wanataka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Chile Arturo Vidal, 32, kwa mkopo. (Mundo Deportivo)Arturo Vidal
Man United wapo ukingoni kukubali mapatano ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Tottenham na Uhispania Fernando Llorente, 34. (Gazzetta dello Sport - via Star)

Lille wanaamini kuwa watafanikiwa kumng'oa kiungo Mreno Renato Sanches, 22, kutoka Bayern Munich. (L'Equipe)
Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer ataweza kutumia kitita cha pauni milioni 75 kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari. Fedha hizo United walizipata baada ya kumuuza mshambuliaji raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, katika klabu ya Inter Milan mwanzoni mwa mwezi huu. (Talksport)

Kiungo Mreno wa klabu ya Leicester City Adrien Silva, 30, amesafiri kuelekea Monaco kwa ajili ya vipimo vya kiafya vitakavyofanyika leo Ijumaa. Silva anatarajiwa kujiunga na Monaco kwa mkopo. (Daily Telegraph)Willy Caballero
Kipa wa Chelsea Muargentina Willy Caballero, 37, anatakiwa na klabu Real Madrid. (Marca - in Spanish)

Ujumbe wa wawakilishi wa Real Madrid upo Ufaransa kufanya majadiliano juu ya uhamisho wa mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27 kutoka klabu ya Paris St-Germain. (Marca - in Spanish)Miamba ya Uhispania klabu za Real Madrid na Barcelona zinagombea saini ya Neymar kumng'oa PSG.

Winga raia wa Brazil anayekipiga na klabu ya Chelsea Kenedy, 23, anaangalia uwezekano wa kuihama moja kwa moja klabu hiyo kabla ya dirisha la usajili la ulaya kufungwa wiki ijayo. (Goal)

Miamba ya Uturuki klabu ya Fenerbahce imejitenga na harakati za uhamisho wa beki wa Manchester United na Argentina Marcos Rojo, 29. (Star)Fenerbahce wanasema hawataki tena kumsajiri mlinzi Rojo (katikati) kutoka Man United

Ombi la Barcelona la kumnunua kwa mkopo wa dau la £137m pamoja na kumpatia kandarasi ya kudumu mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, limekataliwa na PSG huku mabingwa hao wa ligue 1 wakiitisha dau la £229m. (Marca)

Manchester United imemfanya winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19, lengo lao kubwa katika uhamisho wa mwezi Januari na wanajiandaa kutoa dau la £100m. (Sun)
Liverpool, Manchester City, Manchester United, Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa klabu kuu barani Ulaya zinazomlenga mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20, ambaye ana thamani ya £91m. (Sport1 - in German)

Tottenham imeanza mazungumzo ya kumuuza kiungo wa kati wa Kenya Victor Wanyama, 28, kuelekea klabu ya Bruges kwa dau la £11m.
Beki wa Liverpool na raia wa Croatia asiyehitajika sana Dejan Lovren, 30, anaivutia klabu ya Ujerumani ya Bayer Leverkusen baada ya kufeli kupata uhamisho kuelekea Roma. (Bild - in German)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Michy Batshuayi, 25, anataka kusalia na kupigania nafasi yake Chelsea lakini ataitazama hali mwezi Januari. (Standard)

Manchester City inachunguza hali ya kiungo wa kati wa Argentina na klabu ya Velez Sarsfield Argentine Thiago Almada, 18, ambaye bado hajaandikisha upya kandarasi yake na klabu hiyo. (A Bola, via Manchester Evening News)
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post