Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt Ally Mohamed Shein Anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika mkutano mkubwa wa 50 wa chama cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola, Kanda ya Afrika .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Agosti 22,2019, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai amesema wageni mbalimbali wamealikwa ikiwemo Maspika kutoka nchi wanachama,Manaibu Spika,Wabunge na Mabalozi kutoka nchi wanachama waliopo hapa nchini Tanzania watahudhuria pia.
Aidha, Ndugai amesema wanategemea mkutano huo utaingizia nchi kipato kwa maana ya fedha za kigeni, huku akisema kutakuwa na faida kwa wafanyabiashara wao watakao toa huduma kama vile, wamiliki wa hoteli watakapolala wageni,wauza vyakula yaani wauza migahawa na mahoteli bila kusahau eneo maarufu la forodhani.
Kwa upande wake Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai amesema wageni wanatarajiwa kuanza kuingia tarehe 28 agost mpaka tarehe 31 agost.
Mkutano huo wa chama cha mabunge wa chama cha jumuiya ya madola kanda ya afrika ‘’The Commonwealth Pariamentary Association Afrika Region ‘’ hufanyika kila mwaka kwenye nchi wanachama wa chama hicho na kwa mwaka huu mkutano huo utafanyika hapa chini Tanzania, visiwani Zanzibar katika hoteli ya Madinat Al Bahr Kuanzia Agost 31 hadi Tarehe 5,Septemba,2019.
Mwaka jana mkutano huo ulifanyika Gabarone na walishiriki zaidi ya watu mia nne (400),hivyo wanategemea kupata idadi zaidi ya hiyo kwa kuwa waheshimiwa kutoka nchi mbalimbali wameonyesha nia kubwa ya kushiriki
Social Plugin