Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMAA MATATANI KWA KUREKODI VIDEO ZA UCHI WANAWAKE 550

Mwanaume mmoja amekamatwa jijini Madrid akishukiwa kuchukua video za uchi za wanawake zaidi ya 550 kinyume cha sheria.

Mwanaume huyo ana miaka 53 na ana asili ya Colombia, amerekodi video kupitia simu yake ya mkononi aliyoificha kwenye begi lake la mgongoni.

Polisi wamesema kuwa alizirusha mtandaoni video 283 katika tovuti za ngono na zikapata mamilioni ya watazamaji.

Wengi wa walengwa wa video hizo, baadhi ni watoto chini ya umri wa miaka 18, walilengwa maeneo ya usafiri wa treni.

Mwanaume huyo anashukiwa kuchukua video hizo tangu mwaka jana ambapo alianza kuziweka katika mitandao.

Alikua akirekodi pia katika maeneo kama masoko ya kisasa, kuna wakati alikua akijitambulisha kwa walengwa wake ili aweze kupata video nzuri.

Polisi walianza kumfatilia na kumkamata akirekodi mwanamke mmoja kwenye treni.

Katika video iliyowekwa katika mtandao wa Twitter , polisi wamemtaja kama mtu hatari zaidi kwa uhuru wa wanawake

Polisi walifanya upekuzi nyumbani kwake na kukuta kompyuta ikiwa na video zaidi ya mia moja, tovuti yake ina watumiaji 3,519.

Mshukiwa huyo bado anashikiliwa na polisi.

Nchini Uhispania kurekodi video za uchi bila ruhusa ni kosa la kijinsia kisheria na washatkiwa huweza kuhukumiwa kifungo.

Pia imekua kosa la kihalifu huko Uingereza na wales baada ya kampeni iliyofanywa na mwandishi Gina Martin.e.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com