Dkt. Yusto Mchuruza
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo lisilo la liserikali KADETFU na mmiliki wa Redio ya kijamii Kagera Community Radio,Dkt. Yusto Mchuruza amejitolea kuhamasisha wawekezaji kutoka nje ya nchi kwenda kuwekeza mkoani Kagera na kuzijua fursa zilizopo Kagera kupitia radio yake kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Dkt. Mchuruza ametoa ahadi hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kusaidia uwekezaji nchini
katika kikao cha wafanya biashara wa nchi za nje na ndani ya Tanzania kilichowajumuisha kwa pamoja viongozi mbalimbali toka nje na ndani ya nchi kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kwa lengo la kujadili na kutathmini mkoa huo katika eneo la kibiashara.
Mkurugenzi huyo akimuahidi Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti kuwa atajitolea matangazo ya kutangaza fursa za uwekezaji kwa kipindi cha mwaka mzima katika chombo chake ili kuitangaza Kagera kuwa sehemu ya uwekezaji kwa mataifa ya nje jambo litakalosaidia wana Kagera kulifikia soko la kimataifa.
"Natamani hata vyombo vya habari vyote mkoani hapa vishirikiane kwa pamoja kuutangaza mkoa wa Kagera kama eneo la kimkakati kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla",alisema.
Aidha alitoa wito kwa wafanyabiashara kuondoa ubinafsi badala yake washirikiane kwa pamoja ili Kagera iwe mfano kwa mataifa ya nje ili pato la taifa likue na Kagera kuweza kufikia viwango vya kimataifa
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo alipongeza juhudi za mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Elisha Marco Gaguti hasa katika ubunifu wa 'Wiki ya Uwekezaji Kagera' kwani tayari wageni toka nje ya nchi wametambua fuRsa zilizopo Kagera.
Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog
Social Plugin