Waasi wa kihouthi nchini Yemen hapo jana walifanya Shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani dhidi ya kisima cha mafuta cha Shaybah nchini Saudi Arabia kinachotoa takriban mapipa milioni moja ya mafuta ghafi kwa siku.
Hilo ni shambulizi la pili la aina hiyo katika sekta hiyo muhimu ya mafuta nchini humo katika siku za hivi karibuni.
Vyombo vya habari nchini humo viliwanukuu maafisa wa serikali ya Saudi Arabia wakisema kuwa uzalishaji mafuta katika kisima hicho haukuathirika Kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali ya Saudia Aramco, imetoa taarifa inayokiri kutokea moto kiasi katika kituo hicho kinachotoa mafuta huko Shaybah.
Waasi wa kihouthi wamefanya misururu ya mashambulizi ya angani yanayolenga maeneo tofauti tofauti ya Saudi Arabia katika miezi ya hivi karibuni.
Mzozo huo nchini Yemen kwa kiasi kikubwa unaonekana kuwa ni vita baina ya Saudi Arabia yenye Waislamu wa dhehebu la Kisunni na Iran yenye Waislamu wa madhehebu ya Kishia.
Social Plugin