Meneja Ugavi wa TBL, Poul Canute akikabidhi vifaa vilivyotolewa na wafanyakazi kwa Afisa Mwandamizi kutoka taasisi ya Her Africa, Asnath Ndosi Wakati wa hafla hiyo,wengine pichani ni wafanyakazi wa TBL
Meneja wa masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi (wa tatu kushoto) Akiongea Wakati wa hafla hiyo.
Maofisa wa taasisi ya Her Africa wakifurahia msaada huo wa kusaidia wasichana kukabiliana na changamoto ya hedhi wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.
Na Cathbert kajuna - Kajunason/MMG.
Wafanyakazi wa kampuni yak Bia Tanzania (TBL Group), chini ya kampuni mama ya kimataifa ya AB InBev, wametoa msaada wa taulo za kike kwa ajili ya kuwasitiri wasichana wanafunzi wanaosoma shule za sekondari kupitia mradi wa kukabiliana na changamoto za hedhi unaoendeshwa na taasisi ya Her Africa.
Hafla ya kukabidhi msaada huo ilifanyika katika ofisi za makao makuu ya TBL zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyakazi maofisa kutoka taasisi ya Her Africa na wafanyakazi wa TBL.
Akiongea wakati wa hafla hiyo, Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi, alisema kuwa msaada huo umetolewa kutokana na michango ya wafanyakazi baada ya kuguswa na changamoto ya vifaa vya hedhi mashuleni kwa wasichana, hususani wanaotoka kwenye familia zenye vipato vidogo na kuwapunguzia uwezo wao wa kufaulu vizuri kutokana na wengine kutohudhuria masomo wanapokuwa kwenye vipindi hivyo.
“TBL tunayo sera ya kujenga ulimwengu maridhawa ambayo inatekelezwa pia na wafanyakazi, ambapo mara nyingi wamekuwa wakijitoa kukabiliana na changamoto za kijamii na sio kwa kutoa pesa tu bali pia wamekuwa wakitoa hata muda wao kushiriki katika kazi za kijamii kama ambavyo wamefanikisha kutoa mchango huu” alisema Mutiganzi.
Kwa upande wake Mwanzilishi mwenza wa taasisi ya Her Africa nchini, Salha Kibwana, alishukuru wafanyakazi wa TBL kwa kulipa kuipa umuhimu changamoto ya vifaa vya Watoto wa kike wa sekondari kujisitiri wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi mashuleni, kwa kutoa msaada huo na amewahakikishia kuwa utawafikia walengwa
“Nawashukuru kwa kujitoa na nina imani tukizidi kuunganisha nguvu tutafanikiwa kusaidia wanafunzi wengi zaidi hususani maeneo ya vijijini” alisema.
Social Plugin