Na Lydia Lugakila Kagera
Baadhi ya wanawake wajane wilayani Misenyi mkoani Kagera waimeomba serikali kuwapa kipaumbele pale zinapotolewa fursa mbalimbali zikiwemo za mikopo na mgawo wa fedha zinazotolewa kwa ajili ya kunusuru kaya maskini ili waondokane na vikwazo wavipatavyo baada ya kuondokewa na waume zao.
Hayo yamebainishwa wilayani Misenyi mkoani Kagera wakati baadhi ya wanawake hao wakizungumzia changamoto na vikwazo vinavyowakumba mara baada ya waume zao kufariki dunia.
Bi Elieth Elieza ni mama wa watoto sita ambaowanaosoma shule na ambao wameacha shule kabisa kutokana na vikwazo mbali mbali ikiwemo uwezo wa kifedha na kielimu vinavyowafanya wanawake hao kutosonga mbele.
Bi Elieza amesema kuwa kabla ya mume wake kufariki hali ilikuwa nzuri lakini kwa sasa vikwazo ni vingi ambapo amedai kuwa, kuna haja kwa serikali na wadau wengine kuwasaidia kwa namna moja hama nyingine kwa kuwapa vipaumbele ili kuwasaidia kuondokana na vikwazo hivyo pale wanapoondokewa na waume zao.
”Kwa niaba ya wenzangu naiomba serikali itusaidie kutupatia kipaumbele katika fulsa mbali mbali na kututatulia vikwazo vilivyopo",alisema.
Alitaja vikwazo vingine vinavyowakwaza amesema,wajane wamekuwa wakikosa stahiki zao ikiwemo miradhi, mila na desturi zinazowakandamiza wanawake hao wajane huku wakitaja ndugu wa mume kuwa kikwazo pale mume anapofariki dunia kwani hudhurumiwa mali.
Pia ameiomba serikali iwasikilize hasa pale mashtaka yao yanapofikishwa mahakamani ili yapate suluhisho ili kunusuru mali za watoto wanaokuwa wameachwa na wazazi zao.
Hata hivyo Bi Elieza ametaja changamoto kubwa aliyokumbana nayo tangu mwaka 2014 pale ndugu wa mume walipotaka alithiwe na ndugu wa mume wake.
Social Plugin