Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo amewaita Wakuu wa Mikoa (RAS) na Makatibu Tawala wa mikoa (RAS) kwenda jijini Dodoma.
Pamoja na Ma RC, RAS kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara, Waziri Jafo amewaalika wadau wengine kuhudhuria mkutano wa kazi na viongozi hao wenye lengo la kutoa tangazo la uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019.
Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Alhamisi Agosti 22,2019 na Katibu Mkuu wa Tamisemi, Joseph Nnyamhanga amesema Waziri Jafo atatumia huo kutoa maelekezo mbalimbali kuhusu uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Novemba 2019.
Social Plugin