Majeruhi wanne kati ya 43 wa ajali ya Lori lililolipuka Morogoro waliohamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamefariki na kufanya idadi ya waliofariki kufika 75 huku 39 waliobaki wakiendelea kupatiwa matibabu.
Taarifa hii imetolewa na mkuu wa kitengo cha Habari na mawasiliano Muhimbili Bw.Aminiel Aligaesha.
Kuhusu hali za majeruhi mkuu huyo wa kitengo cha mawasiliano amesema wanaendelea vizuri na wapo wanaoonyesha matumaini.
“Tumepoteza wenzetu wengine wanne na miili yao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hivyo kama kuna ndugu wa karibu waje kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao,” amesema Aligaesha.
Social Plugin