Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Wananchi wa kata ya ibihwa wilayani bahi wametakiwa kutowaficha watoto wao ndani kwa kigezo cha ulemavu ,Kama sheria ya mtoto kifungu cha 8 inavyotoa katazo la jamii kumnyima mtoto haki ya kusoma kwa kigezo cha ulemavu.
Akizungumza katika mkutano wa wanachi uliyoratibiwa na shirika la International Aids service jana mkoani Dodoma meneja wa shirika hilo Alan Kamnde alisema ukosefu wa elimu kwa wanachi kuhusu umuhimu wa kumthamini mtoto mwenye ulemavu bado ni kikwazo kikubwa katika jamii.
“Lengo la shirika hili ni kuhakikisha jamii inafikiwa na kupewa uwelewa kuweza kuwaruhusu watoto kupata haki ya kielimu na Zaidi kuweza kuwajumisha watoto wenye ulemavu na wasiyo na ulemavu kujumika na kupata elimu pamoja kwasabau watoto wote ni sawa”Alisema kamnde.
Naye afisa mradi wa shirika hilo Jane Mjidange amesema ni vyema wazazi wakawapenda watoto ,samabmba na kuomba mamlaka zinazohusika kuyashughulikia matukio ya watoto wenye ulemvu kuyachukulia uzito matukio yao.
“Jamani mama zangu hakuna mtoto aliyeomba mungu amuumbe akiwa mlemavu hivyo msiwatenge na ni vizuri hata zile mamlaka zinazohusika zikachukulia uzito kesi za watoto”alisema jenipha.
Diwani wa kata ya Ibihwa, Daudi lesaka alisema katika kata yake kumekuwa na mimba za mara kwa mara kesi zimefikishwa mahakani na zinafanyiwa kazi kwa mujibu wa sharia
Aliongeza kwenye kata yake atachukua hatua kwa familia zote aambazo zimezuia kuwapeleka watoto shule
“Kuhusu swala la mimba tumechukua hatua za kuzipeleka kesi zote mahakamani na zinzshughulikiwa na kwa upande wa familia ambazo zimeshindwa kuwapeleka watoto shule nao tutawachukulia hatua haraka sana” alisema lesaka.