Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANANCHI MKOANI KAGERA WAHIMIZWA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO YA KILIMO ILI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.

Wananchi mkoani Kagera wamehimizwa kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Bi Saada Malunde kwenye kilele cha kufunga maadhimisho ya siku ya wakulima na wafugaji nane nane yaliyofanyika katika viwanja vya Kyakailabwa kata nyanga mkoani Kagera.

Bi Saada amesema kuwa ili kufikia uchumi wa viwanda ni lazima wananchi wafanye kazi kwa bidii ikiwemo kulima mazao ya kilimo, mifugo pamoja na kuendelea kushiriki katika maadhimisho ya siku ya wakulima kila mwaka.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera  Luteni Kanaly  Michael Mtenjele amewashukuru wananchi wote walio jitokeza katika maadhimisho hayo na kuwaomba kuongeza uzalishaji katika mazao.

Sanjali na hayo mh Mtenjele ameongeza kuwa elimu aliyoipata katika maadhimisho ya mwaka huu ataichukua katika wilaya yake ili kuongeza uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com