Kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchini Tanzania,Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri
Na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura mkoa wa Shinyanga lililotakiwa kuanza Agosti 26,2019 hadi Septemba 1,2019 , limeahirishwa baada ya kudaiwa kutokea kile kimeitwa matatizo ya kiufundi na kusababisha kusogezwa mbele.
Akizungumza na Malunde1 blog Msimamizi wa Uchaguzi mkoani Shinyanga Amos Machilika, ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Utumishi na Utawala mkoani Shinyanga amesema zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoa wa Shinyanga litafanyika kuanzia Septemba 2,2019.
“Zoezi la maboresho ya uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura mkoani Shinyanga lilikuwa lianze Agosti 26,2019, lakini kuna matatizo ya kiufundi ambayo yamejitokeza ndipo ikabidi zoezi hili tuliahirishe na kulisogeza mbele ambapo litafanyika kuanzia Septemba 2 mwaka huu” amesema Machilika.
Alhamis Agosti 15,2019 Kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchini Tanzania,Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri akizungumza katika mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi mkoani Shinyanga kikiwa na lengo la kupeana taarifa kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, alitangaza zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura lifanyike Agosti 26 hadi Septemba 1,2019.
Aliwataka watu wenye sifa ya kujiandikisha wajitokeze kwa wingi ili waandikishwe na wanaohitaji kuboresha taarifa zao wakati wa zoezi hilo.
Social Plugin