Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATUMIAJI WA HUDUMA YA MAJI KAHAMA WALIA NA BEI MPYA YA MAJI

SALVATORY NTANDU

Mamlaka ya maji safi na Usafi wa mazingira mjini Kahama (KUWASA) imetakiwa kutumia njia shirikishi wanapotaka kupandisha bei Ankara maji ili kupunguza malalamiko kwa watumiaji wa huduma hiyo pindi bei mpya zinapoanza kutumika.

 Baadhi ya watumiaji wa maji wilayani humo wamesema (KUWASA) wamepandisha Ankara za maji kutoka shilingi 1688 kwa uniti moja hadi  shilingi 1888 kwa uniti moja bila kuwashirikisha.

Wamesema awali kabla ya akra za maji haziongezeka walikuwa wakilipa  shilingi 1015 kwa uniti moja, lakini hapo baadae zikaongezeka hadi  shilingi 1688 nakuongeza kwa mwaka huu wa fedha 2019/20 wameongeza tena hadi kufikia kiasi cha shilingi 1888.

Rajabu Shabani ni mmoja wa watumiaji wa maji kutoka kata ya kahama mjini  amesema ,hawakatai kuongezeka kwa bili za maji lakini mamlaka ya maji ilipaswa kutoa taarifa kwa wananchi ambao ndio wadau wa maji kabla ya kuanza kutumia kwa bei mpya iliyoongezeka ili kupunguza malalamiko.

Amesema Mwaka jana Mamlaka hiyo ilipandisha  Ankara  za maji kutoka  shilingi 1688 na tulikubaliana nayo japo tulilalamika kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa,chakushangaza kabla yakuisha kwa mwaka huu wameongeza tena hadi kufikia kiasi cha shilingi 1888 sawa na ongezeko la shilingi 200.

Sophia Hamisi mkazi wa Malunga nae amesema bei hiyo ni kubwa na inaweza kusababisha wakazi wengi wakaacha kutumia maji kutoka mamlaka hiyo na kuanza kutumia maji ya visima jambo ambalo linaweza likasababisha wakakosa wateja na kupunguza mapato ya taasisi hiyo.

Akijibu Malalamiko hayo Mwenyekiti wa bodi ya kuwasa Meja mstaafu, Bahati Matala amekiri kuongezeka kwa bei hiyo nakuongeza ongezeko hilo linatokana na kikao cha wadau wa maji kiliketi mwaka jana na kukubaliana kuongeza kwa bei ili kutanua mtandao wa maji kwa wananchi.

Amesema kuwa, hapo awali kabla ya kuongeza kwa bei wananchi walikuwa wanatozwa shilingi 1015 kwa uniti moja na ikaongeza hadi kufikia shilingi 1688 na mwaka huu wa fedha 2019/20 bei imeongezeka hadi kufikia kiasi cha shilingi 1888.

Hivi karibuni  Waziri wa maji, Prof.Makame Mbarawa alifanya ziara wilayani kahama  na kuitaka mamlaka hiyo kukusanja mapato ya maji pamoja na kuongeza mtandao wa maji kwa wananchi wa kata 20 zilizopo mjini kahama ampapo kwa sasa kata 12 pekee ndizo zenye huduma hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com