Kaimu Afisa uvuvi wilayani Muleba mkoani Kagera Maengo Nchimani
Na Lydia Lugakila -Malunde1 blog
Kaimu Afisa Uvuvi wilayani Muleba mkoani Kagera Maengo Nchimani ametoa onyo kali kwa wananchi wanaojihusisha na vitendo vya uvuvi haramu vinavyosababisha kipato cha mkoa wa Kagera kushuka.
Nchimani ametoa onyo hilo wakati akiongea na baadhi ya wafanyabiashara waliojitokeza katika uwanja wa Gymkana katika Manispaa ya Bukoba ambako imefanyika wiki ya uwekezaji Kagera yenye lengo la kutangaza fursa mbalimbali zilizopo mkoani Kagera.
Afisa huyo amesema vitendo vya uvuvi haramu vinavyoendelea katika baadhi ya maeneo wilayani Muleba mkoani hapa vinakwamisha maendeleo na jitihada za mkuu wa mkoa wa kagera Brigedia Jenerali Elisha Marco Gaguti za kuutangaza mkoa wa kagera kama sehemu ya uwekezaji ambapo wahitaji wa mazao hayo ya samaki kutohitaji samaki waliokosa ubora na thamani.
Amesema kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo huku akitaja kuanzisha doria za usiku ili kuwabania wale wote wanaofanya vitendo hivyo .
Akielezea wilaya hiyo amesema kuwa wilaya ya Muleba ina zaidi ya mitumbwi zaidi ya 400 na inavua dagaa kwa wingi na uzalishaji wake ni kwa asilimia kubwa hivyo amewataka wananchi hao kuacha tabia hiyo mara moja ili kupata wawekezaji wengi toka nje ya nchi.
Amesema kuwa wilayani hiyo ina changamoto ya kutokuwa na kiwanda cha kuongeza thamani ya zao hilo hivyo kuwataka wawekezaji kujitokeze kwa wingi ili kuinua uchumi wa Kagera .
Amesema juhudi kubwa za utoaji elimu juu ya uvuvi haramu zinafanyika ili kunusuru kizazi cha samaki kwa pato la kagera na taifa zima.
Social Plugin