Wazee sita wenye umri wa kuanzia miaka 62 hadi 85 wamekamatwa na polisi baada ya kukutwa wakifanya mapenzi kwa kuchangia mwanamke mmoja hadharani.
Wazee hao, wanaume watano walikamatwa wakifanya mapenzi na mwanamke pekee mwenye umri wa miaka 85.
Mume wa mwanamke huyo naye alikuwa kwenye kundi la wanaume watano walioshiriki mapenzi hadharani.
Kwa mujibu wa polisi watuhumiwa hao ni Daniel Dobbins(67)OttoWilliams(62), Charles Ardito(75), John Linartz (62), Richard Butler(82) na mkewe JoyceButler (85).
Watuhumiwa hao walikamatwa wakifanya uhalifu huo kwenye Hifadhi ya Grace Richardson iliyopo mji wa Fairfield na wamefunguliwa mashitaka kwa kufanya vitendo vyenye kuvuruga amani.
Hata hivyo, watuhumiwa wote hao waliachiwa kwa dhamana baada ya kuahidi kufika mahakamani wenyewe.
Dobbins aliwahi kukamatwa 2017 baada ya polisi kupata taarifa za kuonekana akitembea uchi kwenye hifadhi nyingine.
Polisi walipofika eneo la bustani walimkuta Dobbins akiwa uchi kwenye gari yake na walipomuhoji alidai anafanya hivyo kwa lengo la kupata tiba.
Social Plugin