Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amesema uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika Novemba 24, 2019.
Jafo ametangaza tarehe ya uchaguzi huo leo Ijumaa Agosti 23, 2019 wakati wa mkutano wake na wakuu wa mikoa, makatibu tawala na wadau mbalimbali uliolenga kutoa maelekezo na tangazo la uchaguzi huo.
Amesema kuwa tangazo hilo ni kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ibara ndogo ya 4,1 hadi 3 chini ya tangazo la serikali number 371 na kuendelea huku akisisitiza muhimu elimu ya mpiga kura kutolewa kwa wakati.
Amesema kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi uandikishaji wapiga kura utaanza siku 47 kabla ya siku ya uchaguzi na utadumu kwa siku saba.
Amesema upigaji kura utaanza saa 2.00 asubuhi na kuhitimishwa saa 12.00 jioni.
Waziri Jafo amesema viongozi watakoma uongozi wao siku saba kabla ya siku ya kuchukua fomu za kugombea.
Amesema waangalizi wa uchaguzi wataruhusiwa baada ya kupata kibali kutoka kwa katibu mkuu Tamisemi na maombi yatatakiwa kupata kibali kwa katiba mkuu ndani ya siku 21 baada ya tangazo la uchaguzi kutoka.
Amesema kampeni sitafanyika siku saba kabla ya tarehe ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi kutoa tangazo hilo katibu mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamuhanga amesema kanuni zote za uchaguzi zimekamilika hadi sasa.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakuu wote wa mikoa nchini mkuu wa mkoa wa singida Dkt.Rehema Nchimbi amesema wako tayari katika maswala ya kiusalama,ulinzi na Amani sanjari na taarifa sahihi na za wakati kwa watu wote bila upendeleo na ubaguzi na utakuwa uchaguzi wa uhuru ,haki na uwazi.
Wakizungumza mara baada ya tangazo hilo baadhi ya viongozi wa vyama tofauti wamesema kuwa huu ndiyo wakati muafaka wa kujipanga kwaajili ya uchaguzi huo.
Ikumbukwe kila baada ya miaka mitano Tanzania bara hufanya uchaguzi wa serikali za mitaa katika ngazi ya kata ,vijiji na mitaa kabala ya uchaguzi mkuu wa wabunge na rais miezi michache baadaye.
Social Plugin