Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI LUKUVI AOKOA ARDHI YA AJUZA NA KUAMURU ALIPWE FIDIA YA SH. MILIONI 500 NDANI YA MIEZI MITATU


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, ametoa miezi mitatu kwa wavamizi 110 waliovamia eneo la Ajuza Nasi Murio, mwenye umri wa miaka 98, lenye ukubwa wa hekari nane kumlipa kiasi cha sh. milioni 500 kama fidia.


Lukuvi ametoa agizo hilo Jijini Arusha Agosti 28, katika kata ya Sinoni ambapo amesema kila mtu atalipa fedha kulingana na ukubwa wa eneo alilopora.

Amesema serikali imewaonea huruma na kwamba watalipa shilingi 20,000 kwa kila mita moja za eneo.

Waziri amesema ili wavamizi hao waweze kurasimishwa na kuwa wamiliki halali watalazimika kulipa gharama za upimaji pamoja na gharama za kupata hati miliki pamoja na kodi ya ardhi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com