Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene ameziagiza Mamlaka zote za Serikali Nchini kuanzia Mamlaka za Mikoa mpaka mamlaka za Vijiji kuweka utaratibu wa kutumia ardhi kwa ajili ya kuhifadhi misitu ili kuweza kutunza mazingira.
Ameyasema hayo jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 5 wa Kisayansi juu ya utunzaji endelevu wa Mazingira ambapo alikua Mgeni Rasmi.
Amesema kuwa Elimu izidi kutolewa kwa Wananchi ili kuweza kupata uelewa zaidi juu ya maeneo ya uhifadhi wa misitu ambayo yametengwa..
Aliyataja maeneo hayo kuwa ni Serengeti-Ngorongoro, Ziwa Manyara, East Usambara, Jozani Chwaka-Zanzibar na Gombe-Masito-Ugalla.
Alisema kuwa maeneo hayo yametengwa kuwa maeneo ya hifadhi kwa sababu ya ikolojia na bayonuai iliyopo katika maeneo hayo. Kwa sasa maeneno hayo yanapata changamoto kwa kuvamiwa na shughuli za Binadamu hivyo kusababisha uharibifu katika maeneo hayo ya hifadhi.
Alisema kuwa ni vema kila Mtanzania kujua umuhimu wa mazingira na hivyo kuweza kulinda na kuhifadhi maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi, na pale yalipoharibiwa basi parejelezwe kwani kwa kufanya hivyo ni kutunza mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George amefungua Mkutano huo wa 5 wa Kisayansi juu ya utunzaji endelevu wa Mazingira ambao umeandaliwa na Baraza la Usimamizi wa hifadhi ya Mazingira (NEMC) na umefanyika katika kumbi za Mikutano za AICC jijini Arusha.
Social Plugin