Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, ameongeza siku tatu kuendelea kuwepo kwa maonyesho ya sikuu ya wakulima kitaifa (Nanenane), kuanzia kesho Ijumaa Agosti 9, hadi jumapili ya wiki hii.
Waziri Hasunga ametangaza uamuzi huo wakati akiongea kwenye kilele cha maonyesho hayo mbele ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Hasunga amesema kuwa uamuzi huo unatokana na wakuu wa mikoa ya Mara, Shinyanga na Simiyu ambao ndiyo waandaji wa maonyesho hayo kanda ya Magharibi kutaka kuongezewa muda.
“Nilipokea ombi la wakuu wa mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga ambao ndiyo waaandaaji wa maonyesho haya, wakitaka kuongezewa siku, nami kwa mamlaka niliyopewa nimekubali ombi lao na kuongeza siku tatu hadi jumapili ya wiki hii ndiyo yamalizike,” amesema Hasunga.
Social Plugin