Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WIZARA MBILI ZASHAURIWA KUSHIRIKIANA KUSAKA MASOKO

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Naibu waziri wa Viwanda, na biashara ,mhandisi Stela Manyanya amesema, wizara yake  kwa kushirikiana na Wizara ya  kilimo  ni muhimu kutafuta masoko kwa wakulima  Mhandisi Manyanya amesema hayo katika mwendelezo wa maonesho ya  wakulima na Wafugaji  kanda ya kati ,Nanenane  ambapo amesema wizara ya viwanda  pamoja na Wizara ya kilimo lazima zishirikiane ili kuleta tija kwa wafugaji na wakulima.


Hivyo,Mhandisi Manyanya amesema Wizara ya viwanda isiposhirikiana na wizara ya kilimo ,Wakulima hawawezi kufanikiwa hivyo lazima wizara yake ya Viwanda iwajibike kutafuta masoko ya wakulima ili waweze  kunufaika na mazao yao.

Aidha,ili kuhakikisha vikwazo hivyo ,serikali imechukua hatua, ya kuunganisha taasisi mbalimbali zilizokuwa zikifanya kazi hiyo,pamoja na kuondoa baadhi ya majukumu ili kuleta ufanisi zaidi katika sekta ya kilimo ,sekta ya mifugo pamoja na sekta ya viwanda.

Maenesho ya wakulima na wafugaji,Maarufu Nanenane yanaendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo kilele chake ni Kesho Agosti 8,2019 huku   kitaifa yakifanyika Mkoani Simiyu na kaulimbiu  kwa mwaka 2019 ni “Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi”


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com