Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA ARDHI KWA KUSHIRIKIANA NA TAKUKURU YAUNDA TUME YA UCHUNGUZI DHIDI YA WATUMISHI 183

Na.Faustine     Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, WILIAM LUKUVI, amesema Wizara hiyo imeunda timu  ya uchunguzi ambayo itakuwa chini ya TAKUKURU, ikijumuisha vyombo vya ulinzi na usalama, kuwachunguza watumishi 183 waliosimamishwa kwa kuingilia mfumo wa kukadilia na kukusanya kodi ya pango la ardhi.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari, kutolea ufafanuzi juu ya kusimamishwa kwa watumishi 183 wa wizara hiyo amesema serikali ilitilia shaka mfumo huo  na kufanya uhakiki.

Uhakiki huo wa miezi sita umebaini kuna watu walitakiwa kulipa kiwango  cha kodi ya pango lakini  kiwango kilichoingia hazina ni kidogo ukilinganisha na kiwango kilichofutwa katika mfumo wa malipo ikionesha kiwango hicho kimelipwa.

Amesema kutokana na matokeo ya uhakiki huo Wizara kupitia kwa katibu Mkuu wa Wizara hiyo wanaunda timu ambayo itakuwa chini ya TAKUKURU na vyombo vingine vya usalama kuchunguza jambo hilo na makosa mengine yatakayoonekana katika uchunguzi huo.

Waziri Lukuvi ametumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi hususan Wa wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na Mkoani Mtwara  kwa kuonesha  ushirikiano wa kutoa taarifa dhidi ya watumishi wa ardhi waiokuwa waaminifu.

Aidha waziri Lukuvi amewatoa hofu wana nchi kutokana na idadi kubwa ya maafisa ardhi waliosimamishwa amesema Shughuri za kiserikali katika Ofisi hizo zitaendelea kama kawaida.

Pia amewataka wananchi kutumia mfumo wa kielecronic kulipia kodi ya pango ili kuepusha vitendo vya rushwa, na amesema kwa wale wote ambao fedha za malipo ya pango zilifutwa bila malipo kuonekana katika mfumo na wale ambao yameingia malipo pungufu wote watalipa kiasi kilichobaki kukamilisha malipo hata kama wamelipa.

Hata hivyo,Waziri Lukuvi ametolea Mfano suala la Mmiliki wa  Mbeya Hotel ambapo alipunguziwa ukubwa wa eneo  lililokuwa na Ukubwa wa Mita za Mita za mraba 20,234 lakini kwenye mfumo wa malipo akawa analipia gharama ya   Mita za Mraba  502 badala ya 20,234 tangu mwaka 2002 baada ya kufanyiwa ujanja na mtumishi wa ardhi .

Hivyo alitakiwa kulipa zaidi ya  Tsh.Milioni 6  kwa Mwaka, kutokana na ujanja amepatana na mtu wa mfumo  badala yake wanamtoza zaidi ya 63 elfu pekee tangu mwaka 2002 pekee kwa mwaka na kwa malipo halisi serikali inamdai zaidi ya Tsh.Milioni 68.

Timu hiyo ya Uchunguzi itaanza kufanya kazi kuanzia Wiki ijayo Siku ya Jumanne ambapo itafanya uchunguzi kwa muda wa siku 30.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com