Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA UCHUKUZI YAANZA KUKUSANYA MAONI YA WADAU KUJADILI RASIMU 8 ZA KANUNI ZA USAFIRISHAJI

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Wizara ya ujenzi , uchukuzi na mawasiliano imeanza kukusanya maoni kutoka kwa wadau wa usafirishaji  wa Ardhini nchini,  maoni yatakayosaidia kuboresha rasimu nane za kanuni  zilizoandaliwa na wizara hiyo zitakazo saidia kuondoa baadhi ya vikwazo vya usafiri wa Ardhini.

Akizungumza jijini Dodoma Agosti 28,2019   wakati akifungua kikao hicho kilichowahusisha wadau wa uasafirishaji pamoja na mamlaka ya uasafiri wa ardhini LATRA ,katibu mkuu wa  uchukuzi Dkta Leonard Chamriho amewataka wadau hao kuwa huru katika kutoa maoni yao yatakayosaidia kuleta matokeo chanya katika sekta ya usafirishaji wa Ardhini.

Mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti usafirishaji ardhini (LATRA) Gerald Ngewe amesema kuwa  maoni ya wadau ni muhimu katika urekebishaji wa sera na sheria katika sekta hiyo.

Hata,hivyo amezungumzia  kifungu cha kanuni ya 10 juu ya Masharti ,ambapo yanamtaka mtumiaji wa vyombo vya usafiri kutotumia vilevi,kuvaa sare safi,kutoruhusu watu kufanya biashara ndani ya basi ,kutozidisha abiria pamoja na kuzingatia ukomo wa mwendo kasi.

Nao baadhi ya Wadau wa Usafiri hapa nchini wamesema ni vyema LATRA ikajikita zaidi katika utoaji wa elimu kwa wadau.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com