Marais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda wamesaini makubaliano ya amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda, kumaliza uhasama uliopo kati ya mataifa hayo jirani.
Walifikia makubaliano hayo katika mkutano huo wa pili mbele ya marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Angola na Congo Brazzaville waliokuwa wapatanishi katika mgogoro huo.
Joto la kisiasa limekuwepo tangu mwanzoni mwa mwaka huu na limeathiri maisha ya watu kijamii na kiuchumi katika mataifa hayo jirani.
Maofisa nchini Rwanda wameishutumu Uganda kwa kuwafunga na kuwatesa kinyume cha sheria raia wake nchini Uganda, wakati Uganda nayo inaishutumu Rwanda kutekeleza ujasusi katika ardhi yake.