Na Editha Karlo - Malunde1 blog
ASKARI wawili wa Jeshi la wananchi(JWTZ) kikosi cha 24KJ Mkoani Kigoma,wamefariki dunia na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa katika ajali iliyotokea leo kwenye hifadhi ya Katavi.
Askari hao wamepata ajali baada ya gari la jeshi lililokuwa limebeba silaha kupinduka wakati wakielekea kwenye oparesheni Mkoani Katavi.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni Lameck Mdengo amethibitisha kupokea majeruhi hao pamoja na maiti mbili.
"Ilikuwa majira ya saa 8 tulipokea majeruhi 20 na wawili wakiwa wamefariki dunia ambao tumewapatia huduma ya kwanza,wapo waovunjika mikono na miguu pia lakini tunafanya utaratibu kuwapa rufaa ya kwenda Muhimbili au Bugando",alisema.
Aliwataja waliofariki ni Bakari juma Mohamed,Rashid Abed Mwimbe
Social Plugin